Jump to content

User:Hajimussamrith/sandbox

From Wikipedia, the free encyclopedia

VITA VYA KIMATAIFA

[edit]

Vita ni nini Vita ni mapambano baina ya nchi, mataifa au angalau vikundi vikubwa vya watu yanayoendeshwa kwa nguvu ya silaha.

Mchoro wa Pier Gerlofs Donia na Wijerd Jelckama wakipigana kwa ajili ya uhuru wa watu. Katika vita kuna pande mbili au zaidi. Husababisha mateso, vifo na kuharibika kwa mali ya watu pamoja na mazingira asilia. Mwanamgambo wa Kipalestina akiwa ameshika silaha aina ya M16 rifle, mwaka 2009.

Asili ya vita ilikuwa mapambano kwa silaha kati ya makabila au vijiji mbalimbali. Baada ya kutokea kwa madola ilikuwa zaidi serikali au watawala wa madola walioamua juu ya vita.

Vita Kuu ya Pili ya Dunia

[edit]

Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa vita vya kimataifa vilivyodumu kuanzia mwaka 1939 hadi 1945. Ilihusisha nchi nyingi za dunia zilizogawanyika katika muungano wawili wa kijeshi unaopingana: Washirika, wakiongozwa na Uingereza, Marekani, na Umoja wa Kisovyeti, na Mhimili, wakiongozwa na Ujerumani, Italia, na Japani. Ilikuwa ni vita vikubwa zaidi na vya gharama kubwa zaidi katika historia ya binadamu, vikihusisha zaidi ya nchi 100 na watu zaidi ya bilioni 2 waliojihusisha moja kwa moja katika mapigano. Zaidi ya wanajeshi milioni 80 walipigana, na vifo vya jumla vya kijeshi vilifikia takriban milioni 20 na vifo vya vifo vya raia milioni 25-70. Vifo vingi vya raia vilitokana na njaa, magonjwa, na mauaji ya halaiki.

World War II in Photos

Vita vilianza tarehe 1 Septemba 1939, Ujerumani ilipovamia Poland. Uingereza na Ufaransa zilitangaza vita dhidi ya Ujerumani siku mbili baadaye. Baada ya miezi miwili ya vita vya uwongo, Ujerumani iliuvamia Udenmark na Norway mnamo Aprili 1940, kisha Ufaransa na nchi za chini mnamo Mei 1940. Uingereza pekee ndio ilipinga mashambulizi ya Ujerumani huko Ulaya. Umoja wa Kisovyeti uliungana na Mhimili mnamo Agosti 1939 kwa kusaini Mkataba wa Molotov-Ribbentrop, lakini uliivamia Finland mnamo Novemba 1939 na kuvamia maeneo ya mashariki mwa Ulaya mnamo Juni 1941. Japani, mshirika wa Mhimili, uliishambulia bandari ya Marekani ya Pearl Harbor mnamo Desemba 1941, na kuleta Marekani kwenye vita.

Mnamo 1942, wimbi liligeuka dhidi ya Mhimili. Ujerumani ilishindwa katika vita vya Stalingrad dhidi ya Umoja wa Kisovyeti, na kushindwa kwa Japani katika vita vya Midway kuliashiria mwisho wa upanuzi wake wa Pasifiki. Washirika walianza kusukuma nyuma kwenye nyanja zote. Mnamo 1944, Washirika waliwasili Ufaransa na kuwafukuza Wajerumani. Mnamo Mei 1945, Ujerumani ilijisalimisha, na kumaliza vita huko Ulaya. Mnamo Agosti 1945, Marekani iliangusha mabomu ya atomiki kwenye miji ya Japani ya Hiroshima na Nagasaki, na kusababisha Japani kujisalimisha siku sita baadaye. Vita hivyo vilimalizika rasmi mnamo 2 Septemba 1945, kwa kusainiwa kwa hati ya kujisalimisha kwa Japani.

Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa na athari kubwa kwa ulimwengu. Ilibadilisha ramani ya kisiasa ya dunia, na kusababisha kuongezeka kwa Marekani na Umoja wa Kisovyeti kama mataifa makubwa mawili. Ilileta pia kuundwa kwa Umoja wa Mataifa, ili kuzuia migogoro ya baadaye ya kimataifa. Vita hivyo vilileta mabadiliko makubwa katika jamii na utamaduni, na kusababisha kuongezeka kwa harakati za haki za kiraia na haki za wanawake.

Vita vya Urusi na Ukraine

[edit]

Mzozo kati ya Urusi na Ukraine ulianza Febrauri 2014, ukihusisha vikosi vya wanaotaka kujitenga vinavyosaidiwa na Urusi kwa upande mmoja, na Ukraine kwa upande wa pili. Mzozo huo unahusu hasa hadhi ya Crimea na Donbas.

Msukumo wa kihistoria na tamaduni Ili kuelewa mgogoro huu unaoendelea ni muhimu kuelewa historia ya mahusiano ya nchi hizi pamoja na mwingiliano wa tamaduni kati yao. Historia ya Ukraine na Urusi inaenda miaka mingi nyuma hata kufikia karne ya 17. Lakini kwa uelewa wa haraka tuanzie miaka ya mwanzo ya 1990. Mwishoni mwa miaka ya 1980, Shirikisho la Soviet lilianguka. Shirikisho hili kitovu chake kilikua Urusi. Sovieti ilikua shirikisho la nchi takribani 15 ambazo ni Urusi, Ukraine, Georgia, Belorussia, Uzbekistan, Armenia, Azerbaijan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Moldova, Turkmenistan, Tajikistan, Latvia, Lithuania and Estonia. Na pia kuna nchi zingine ambazo hazikuwa chini ya shirikisho lakini zilikua chini ya utiisho wa Soviet, yaani Soviet akisema ruka wanaruka bila kuuliza, ambazo ni Poland, Romania, Czechoslovakia, Hungary, Bulgaria, Ujerumani ya Mashariki, Yugoslavia na Albania.

Ramani inayoonyesha Shirikisho la Sovieti

Ramani inayoonyesha Shirikisho la Sovieti Mawimbi ya nchi kujitenga na shirikisho la Sovieti yalisambaa miaka ya mwisho ya 80 mpaka mwanzoni mwa 90. Nchi nyingi zikaamua kutangaza uhuru wake. Hizi zinatajwa kuwa ni nyakati kubwa za aibu kwa Urusi ambapo hadhi yake kama ‘super power’ iliondolewa. Kama ilivyo kwa nchi zingine zilizojitenga, Disemba 1, 1991, wananchi wa Ukraine wanapiga kura ya maoni na kuamua kuwa taifa huru.

Hata hivyo, bado Ukraine wanabaki na uhusiano mkubwa na wa muhimu na Urusi. Wakati wa Sovieti sehemu kubwa za silaha za kinyuklia zilikua zinahifadhiwa nchini Ukraine. Mwaka 1994, Ukraine iliamua kujihakikishia mamlaka yake kama nchi huru kwa kutoa silaha zote za nyuklia zilizoachwa na Soviet na kusaini mkataba kwa masharti kuwa Urusi na mataifa mengine makubwa yataheshimu uhuru wake kama nchi.

Mkataba huo uliosainiwa na Urusi, Marekani na Uingereza unajulikana kwa jina maarufu kama Makubaliano ya Budapest. Baadhi ya wachambuzi wenye mrengo mkali wanachukulia hili kama kosa kubwa walilofanya Ukraine.

Ukiacha historia kati ya Urusi na Ukraine, jambo lingine la kuangalia ni mwingiliano wa tamaduni kati ya watu wa Ukraine na watu wa Urusi.

Walau asilimia 20 mpaka 30 ya wakazi wa Ukraine wanaongea Kirusi kama lugha ya kwanza. Lakini majimbo ya Luhansk, Donetski na Crimea ni majimbo ambayo watu wanajitambulisha na kujitanabaisha kama Warusi pia. Crimea ina historia yake ya pekee.

Mpaka mwaka 1954, Crimea ilikua sehemu ya Urusi, yaani pamoja na nchi zote hizi kuwa chini ya Soviet, bado zilikua na mipaka. Kiongozi wa Soviet wakati huo aliamua kuigawa Crimea kwa Ukraine, hasa ikizingatiwa kigeographia Crimea imeungana na Ukraine haijaungana na Urusi.

Ukraine inavyopata uhuru, Crimea inabaki kuwa sehemu ya Ukraine. Tutaona umuhimu wa Crimea, Luhansk na Donetski katika sakata hili mbele kidogo katika makala hii.

Urusi na NATO Nyakati za anguko la Shirikisho la Soviet zinatajwa kama nyakati za aibu kwa taifa la Urusi. Taifa lao liliabika hasa kwa kuwa na kiongozi aliyeitwa ‘mlevi,’ kuanguka kwa heshima yake kama ‘super power’ pamoja na ukata mzito. Toka wakati huo, Urusi imekuwa ikitafuta namna ya kurudisha hadhi na utukufu wake wa mwanzo. Kuingia kwa Putin madarakani mwaka 2000, mwanainteligensia wa zamani aliyeweza kutiisha makundi mbalimbali ndani ya Urusi, pamoja na kufanikiwa kuirudisha Urusi kiuchumi, analeta sura mpya ya urudishaji wa hadhi ya mwanzo ya Urusi. Urusi chini ya Putin inachangamka kwa namna ya kipekee na kuongeza ushawishi ndani na nje ya Urusi. Lakini kuna shida moja kwenye huu muonekano mpya wa Urusi: NATO. NATO, ambao ni umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi ukiongozwa na Marekani, inakuwa mwiba kwa Urusi kwa namna moja au mbili. Umoja huu uliundwa kwa lengo la kukabiliana na Shirikisho la Soviet (Urusi ya zamani). Mataifa mengi yaliyoondoka chini ya Shirikisho la Sovieti kwa kuzingatia udogo walionao mbele ya Urusi, fursa za biashara na kutaka kulinda uhuru wao wanaamua kujiunga na umoja wa ulaya na pia NATO. Hii inajumuisha nchi kadhaa ambazo zimepakana ubavu kwa ubavu na Urusi. Geographia ya Urusi ni tofauti na nchi zingine kubwa ambazo zina mipaka ya kigeographia kama mito na bahari zinazotenganisha nchi na nchi. Kwa Urusi sehemu kubwa ya mipaka yake zimetengwa na ardhi ya nchi zingine. Kwa miaka mingi Urusi imekuwa ikijihakikisha usalama wake kwa kuziweka nchi zinazoizunguka chini ya mbawa zake. Mataifa kama Ukraine na Georgia nayo yanapata msukumo mbalimbali hasa kutoka kwa wananchi wao juu ya kulandana na nchi za magharibi, jambo ambalo Urusi hairuhusu. Kwani kwa nchi hizi kujiunga na umoja wa ulaya au NATO, moja kwa moja zinadidimiza ushawishi wa Urusi. Hata hivyo, nchi hizi ni huru na zina haki sawa sawa na Urusi. Urusi chini ya Putin inajiona imerudisha utukufu wake wa mwanzo. Kuzungukwa na NATO ni kama kumbukumbu mbaya ya nyakati za aibu jambo ambalo tutaona linavyokuwa sababu ya mzozo unaoendelea.

Watu wa Ukraine Baada ya Ukraine kupata uhuru wake na kuamua kuwa nchi ya kidemokrasia inaingia kwenye mabadiliko kadhaa ya mfumo wa kitaifa. Badiliko la kwanza ni badiliko la kiuchumi kutoka uchumi unaohodhiwa na dola mpaka kwenda kwenye uchumi huria. Mabadiliko haya ya kwenda kwenye uchumi huria yanafanywa kwa namna ambayo baadhi ya vikundi vya watu walio karibu ya uongozi ndio wanaokuwa wanufaika wakubwa. Rushwa na ubadhirifu, utekwaji wa dola, ukiukwaji wa haki na kutofwatwa sheria vinagubika uongozi mpya. Kashfa kama ile ya uvujishwaji wa mazungumzo ya Rais Leonid Kuchma yaliyoonesha Rais akitoa maagizo ya mauaji ya mwandishi wa habari aliyekuwa akifichua rushwa Serikali, zinaghubika maisha ya Ukraine mpya. Katika yote haya, viongozi wa Ukraine wanahakikisha wana mahusiano mazuri na uongozi wa Urusi kiasi kwamba hata wananchi wanahoji maswali juu ya uhuru wao kama nchi. Rushwa inawasukuma watu wa Ukraine kutaka kuona mabadiliko. Wanataka kuwa na nguvu juu ya nchi yao na hatma zao. Kumbuka, mfumo wa kiutawala wa demokrasia, au mfumo ambao unawapa nguvu zaidi watu, ni mfumo unaoendana zaidi na nchi za magharibi kuliko kwa upande wa Urusi. Machoni kwa Urusi, hili si jambo zuri kwa mustakabali wa mahusiano kati ya Urusi na Ukraine. Mwaka 2004, katika uchaguzi wananchi wa Ukraine wanaamua kuonyesha nguvu yao. Mawaziri wakuu wawili wastaafu Viktor Yushchenko and Viktor Yanukovych wanagombania uchaguzi. Uchaguzi huu unakuwa na mambo mengi ikiwemo kunywesha sumu kwa mgombea wa upinzani, Viktor Yushchenko, jambo ambalo lilimfanya kunusurika kifo na kubakia na sura iliyoharibiwa kabisa. Huku Urusi na wanainteligensi wa Ukraine wakirushiwa lawama juu ya jaribio hili la kumuaa Yushenko.

Viktor Yushchenko na Yuliia Tymoshenko wakati wa mapinduzi ya Orange
Viktor Yushchenko na Yuliia Tymoshenko wakati wa mapinduzi ya Orange

Kutwaliwa kwa Crimea

Mwanzoni nilikuelezea Ukraine kuna upande hasa Crimea, Donetski na Luhanski. Hawa wanajitambulisha kama Warusi na mara zote hufungamana na Urusi. Wengi wao hata vyombo vya habari wanavyofuatilia ni vya Urusi.

Baada ya kuondolewa kwa Rais wa Ukraine, Urusi inatumia ushawishi wake ndani ya haya maeneo kusambaza taarifa potofu kama Serikali ya Kiev inampango wa kuwamaliza,  na wanatumia habari ya Ukraine kutaka kusaini mkataba wa Umoja wa Ulaya kama chambo.

Hata hivyo, tayari kuna makundi ya watu wanaoipinga msimamo wa wengi ndani ya Ukraine wa kuwa na mahusiano mazito na magharibi kama ilivyo na Urusi. Ghafla katika jimbo la Crimea, wanaibuka watu wenye silaha wanaovalia sare za kijeshi za rangi ya kijani, bila utambulisho wanatokea nchi gani au wana mrengo upi, watu hawa wanapewa jina la ‘little green men’, watu wadogo wa kijani. Watu hawa wanaibuka mwishoni mwa mwezi wa pili wa 2014.

Urusi kuvamia Ukraine

Mpaka mwisho wa mwaka 2021, Urusi imekuwa ikifanya mazoezi na kupeleka silaha na wanajeshi wake katika mpaka wake na Ukraine. Pamoja na kupinga kuwa haitavamia Ukraine, mnamo Februari 24, 2022, Urusi anaingia ndani ya Ukraine.

Rais wa Urusi anasema uongozi uliopo unakandamiza watu na ni wa-kinazi. Lakini baada ya muda anaenda mbali na kusema kihistoria Ukraine iko chini ya Urusi na hatambui Ukraine kama nchi huru.

Wataalamu wengi walitengemea Urusi itachukua muda mrefu kabla ya kujaribu kuteka mji mkuu. Ila siku ya pili tu ya kuvamia Ukraine, Urusi inajaribu kuingia mpaka Kiev. Hii ikimaanisha kwa upande wa Urusi wameshafunga kitabu cha mazungumzo.

Taarifa za kiinteligensia na chambuzi za wataalamu zinahitimisha kuwa lengo la Rais wa Urusi ni kumuondoa Rais waliyepo na kumweka mwingine. Rais wa Ukraine anatoa taarifa kuwa kuna orodha ya watu watakaouliwa ambapo jina lake ni la kwanza, likifuatia na familia yake.

Urusi ina nguvu kuliko Ukraine. Bila msaada wowote wa maana kama inavyoendelea sasa ni wazi kuna uwezekano mkubwa wa Ukraine kudhibitiwa.

Lakini kuna mambo kadhaa yanayofanya isiwe rahisi kihivyo. Kwanza, Ukraine imekuwa katika hali ya kivita kwa muda mrefu. Uwepo wa makundi ya raia waliokua wakijitolea kupigana, kunafanya vita hii iwe ngumu.

Pili, kwa upande wa Urusi wangetaka vita hii imalizike mara moja, hasa kwa wao kushinda. Kwasababu jinsi wanavyokaa ndani ya Ukraine, ndio nafasi ya mambo kuharibika ndani ya Urusi inavyoongezeka. Hali inaonyesha mipango ya Urusi haijaenda jinsi walivyotarajia hasa katika kuuteka Kiev. Huku nyumbani Urusi tayari kuna maandamano yanayotokea hapa na pale na kuna uwezekano wa kupata nguvu zaidi.

Pia, vikwazo vinavyowekwa tayari vinaanza kufanya kazi, ikiwemo kuzuia sehemu kubwa ya mali na viongozi na baadhi ya watu mashuhuri wa Urusi kuingia Ulaya na Marekani na nchi rafiki.

Tayari meli kadhaa za Urusi zinaripotiwa kukamatwa. Ndege ya kiongozi wa Bunge ilirudishwa katikati ya safari. Kubwa zaidi ni vikwazo juu ya Benki ya Urusi, hii itafanya mambo kuwa magumu kwa raia wa Urusi jambo ambalo litaendelea kumweka matatani pia Rais wa Urusi kwa upande wa nchi yake.

Jambo la tatu kufanikiwa kwa kampeni ya Urusi ndani ya Ukraine inamaanisha anaweza kuendelea na nchi zingine zinazozunguka Urusi na zenye historia na Urusi. NATO hawataruhusu kuwe na ushindi wa moja kwa moja katika hili ingawa pia hawataingia katika vita ndani ya Ukraine.

Nchi zingine

Kuna makundi matatu ya nchi zingine katika mgogoro huu zenye maslahi ya moja kwa moja. Kundi la kwanza ni NATO, kundi la pili ni China na kundi la tatu nchi zenye historia na Urusi.

Kwa upande wa NATO wameshatoa msimamo kuwa hawataingiza majeshi ndani ya Ukraine kupigana. Sababu katika hili zinaeleweka. NATO akiamua kuingiza majeshi ndani ya Ukraine, haiwezi kuwa vita ya kawaida tena, ni vita ya nyuklia maana Urusi hatakubali kushindwa na wote wana silaha za nyuklia. Jambo hili Rais wa Urusi amelisisitiza.

Lakini NATO anamaslahi katika hili. Maslahi yake yanakuja na swali kwamba nini kinamzuia Urusi kuendelea na nchi zingine hasa zilizo pembezoni kabisa ya mipaka kama atafanikiwa kampeni yake ya Ukraine?

Upande mwingine ni China, taifa hilo ni mshirika wa karibu na wa kipekee wa Urusi.  Kwanza China anamuhakikishia Urusi kununua gesi yake kama vikwazo vikiendelea kuwekwa. Lakini pia ushawishi wa China ni muhimu. China na Urusi wamekuwa wakikubaliana katika mambo mengi hasa katika kuzuia ongezeko la ushawishi wa marekani duniani na karibu na mipaka yao.

Laini pia mgogoro huu ni picha nzuri kwa China kupima namna mataifa makubwa yanavyojibu katika matukio kama haya. China amekuwa na mgogoro wa kihistoria na Taiwan, ambapo inaiangalia nchi hiyo kama sehemu ya nchi yake huku Taiwan ikijitambulisha kama nchi huru. China kuwa upande wa Urusi ni muhimu sana kwa sasa, na mpaka sasa imeendelea kuhakikishia Urusi juu ya kumuunga mkono.

Tatu, nchi zenye historia ya kuwa chini ya utawala wa Urusi, hasa ambazo ziko pembezoni ya Urusi, zimeanza kuonyesha hofu yake kama Urusi akifanikiwa ndani ya Ukraine basi zenyewe zitafuatia. Nchi za Baltiki (Estonia, Latvia and Lithuania) zimeonyesha hofu hiyo juu ya mgogoro huo.

Kwa sisi wengine nje wa hayo makundi matatu athari kubwa tutakayoiona ni upandaji wa bei za mafuta. Urusi kuwa mmoja wapo wa mzalishaji mkubwa wa mafuta maana yake ni lazima mzozo huu utaathiri usambazaji wa mafuta duniani, hivyo bei kupanda.

Hata hivyo, bado wengi wanaamini mlango wa mazungumzo unaweza ukafunguka tena. Hatua ya hivi karibuni ya nchi za ulaya na marekani kuzuia benki za Urusi kutumia mfumo wa kibenki wa swifti pamoja na NATO kuongeza majeshi karibu na mipaka ya Urusi inaweka shinikizo zaidi kwa Urusi kurudi kwenye mazungumzo.