Jump to content

User:Mwalimu nassoro

From Wikipedia, the free encyclopedia

Jina la Kiraia/Kamili Mwalimu Nassoro Athumani Uraia Tanzania Jinsi Me Kuzaliwa Septemba 19, 1980 Kabila Zaramo Kazi Mwalimu Shughuli binafsi Biashara/Mjasiliamali


Mwalimu Nassoro Athumani alizaliwa Septemba 19,1980 katika wilaya ya Ilala jijini Dares-Salaam. Ni mtoto wa pili kuzaliwa kwa upande wa mama na ni wa tatu kuzaliwa kwa upande wa baba. Mzee Nassoro Athumani Mohammed alikuwa ni muajiriwa benki ya CRDB na mama yake mzazi anayeitwa Mkejina Mwalimu Kinyogoli ni mwajiriwa serikalini makao makuu ya jiji la Dares Salaam (Dares-Salaam City Council).

Elimu: Mwalimu Nassoro alianza elimu yake ya msingi mnamo mwaka 1991 Shule ya msingi Marumbo iliyopo kijijini Marumbo, wilayani Kisarawe- Pwani na kuhitimu darasa la saba mwaka 1997. Baada ya elimu yake ya msingi alijiunga na chuo cha mafunzo ya kingereza na komputa (Desemba 1997) kiitwacho Dares Salaam English and Computing center ambapo alihitimu March 1998. Januari 1998 aliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari St. Mathew iliyopo Kongowe Mbagala (Pwani) ambapo alisoma kwa miezi sita tu toka januari 1998 hadi julai 1998 na baada ya hapo August 25, 1998 alihamia shule ya sekondari Airwing inayomilikiwa na Jeshi la Anga la Tanzania katika jiji la Dares Salaam ambapo alihitimu 2001. Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 2002 alijiunga na elimu ya kidato cha tano Makongo Sekondari shule inayomilikiwa na jeshi la ulinzi la Tanzania (TPDF) na kuhitimu kidato cha sita 2005 ambapo ni mwaka huo huo aliohitimu mafunzo ya cheti cha teknolojia ya kopyuta kutoka Compware Training center kilichopo Dares Salaam. Mwaka 2005 Mwalimu Nassoro Athumani alijiunga na elimu ya chuo kikuu ambapo alichukua shahada ya kwanza ya elimu (BA Education) Kampala International University jijini Kampala nchini Uganda na kuhitimu mwaka 2008.

Kazi: Baada ya kuhitimu kidato cha sita alibahatika kufanya kazi akiwa kama statistics surveyor/supervisor katika mradi wa mabasi yaendayo kasi jijini Daressalaam ujulikanao kama DART(Dar Rapid Transit). Mwaka 2009 aliajiliwa na kampuni iitwayo FUGALIMA LIMITED akiwa kama Programs manager na pia wakati huo huo alikuwa akifanya kazi katika kampuni iliyoitwa FIRST FORTUNE LIMITED akiwa kama Company Coordinator. Baadae aliamua kuacha kazi katika kampuni hizo na kupata part time ya kuandaa taarifa ya machapisho katika gazeti la Tanzania Daima ambapo alidumu nayo kwa miezi michache kabla ya kuacha. Kwa sasa Mwalimu Nassoro ni mwalimu wa sekondari katika shule ya sekondari Mbemba iliyopo Masasi Mtwara na pia ni mjasiliamali. Mwalimu Nassoro pia aliwahi kufundisha shule za sekondari GoldMax High school na St. James sekondari zote zilizopo nchini Uganda.