Jump to content

User talk:Rwebangira

Page contents not supported in other languages.
From Wikipedia, the free encyclopedia

SIMONI WA KIRENE

[edit]

Katika Biblia inaonekana SIMONI WA KIRENE alimsaidia Yesu kubeba Msalaba. Mbona hakuna andiko linaloonesha alimrudishia Yesu ule Msalaba? Yeye nadhani ndio alisulubiwa Yesu!!

Jibu Fupi: Waliubeba Msalaba pamoja-Simoni Mkirene nyuma yake Yesu (Lk 23:26). Hakuna andiko linaloonesha SIMONI WA KIRENE alimrudishia Yesu Msalaba wake maana Waliubeba pamoja. Kwa nyongeza, si Kila jambo kumhusu Yesu limeandikwa katika Biblia (Yoh 21:25), yaliyoandikwa ni ili tumaini,na Kama yangeandikwa yote, hakuna kitabu kingeweza kutoshelezea. Kwamba SIMONI Ndiye aliyesulubiwa si Yesu; huo ni uongo mkubwa maana Yesu mwenyewe alishatabiri kuhusu yatakayompata( Mt 26:61, 27:40) naye Pilato aliweka hati katika Msalaba iliyothibitisha ni Yesu aliyesulubiwa (Mt 27:37, Yn 19:19). Rwebangira (talk) 09:56, 2 March 2023 (UTC)[reply]

Ahsante Sana Rwebangira (talk) 10:27, 2 March 2023 (UTC)[reply]

KUHUSU YALIYOMPELEKA YESU KUZIMU

[edit]

Yesu baada ya kufa siku ya ijumaa alienda kuzimu.Kwa mujibu wa mafundisho ya Kanisa,alienda kufanya Nini huko? JIBU( REJEA KKK Na: 631-637) Kuzimu ni pande za chini za nchi, ambazo ni makao ya wafu(Ef 4:9-10,Hes 16:33). Ni kweli Yesu baada ya kufa alikwenda kuzimu,akakaa huko kabla ya kufufuka (Rej.Mdo 3:15; Rum 8:11; Ebr 13:20). Sasa Yesu alienda kufanya Nini huko kuzimu? Alienda kufanya yafuatayo:

(i) Kutangaza habari njema kwa zile roho zilizofungiwa kule (1pet 3:18-19,4:6; Yoh 5:25; Ef 4:9; KKK 632). Yesu hakwenda kutoa hukumu (KKK 633; Mt 27:52-53)!

(ii) Kuokoa Roho Takatifu zilizokuwa zikimgonjea Mwokozi; yaani zile roho zilizokuwa na haki mbele za Mungu (Rej.Mt 27:52-53; KKK 633; Katekismu ya Kirumi Na: 1, 6, 3). Rwebangira (talk) 10:18, 2 March 2023 (UTC)[reply]

KUHUSU CHEO CHA UKARDINALI

[edit]

Kardinali ni nani katika kanisa Katoliki? JIBU: Rejea MSK 349-359

โ€ขKardinali ni kiongozi katika Kanisa Katoliki,ambaye anateuliwa na Papa (MSK 351) mwenyewe na huwa na kazi kuu mbili: kumshauri Papa na Kumchagua Papa (MSK 353,355). Kardinali aliyetimiza miaka 75 hupaswa kuandika barua ya Kuomba kustaafu kwa Baba Mtakatifu (MSK 354) Rwebangira (talk) 10:42, 2 March 2023 (UTC)[reply]

KUHUSU RUHUSA YA TALAKA

[edit]

Shutuma: Biblia imeruhusu wanandoa kupeana TALAKA (Rejea Mt. 19:9) kama ni Kwa kosa la uasherati. Lakini Wakatoliki hawatoi ruhusa hii.

โ€ขJibu 1: Kifungo Cha ndoa hakifunguki (Mw 1:27; 2:24). Yesu anaposema " isipokuwa ..." hataki kutoa ruhusa ya kufungua na kufunga ndoa nyingine kwa halali .Hata katika ugoni, ruhusa kama hiyo haipatikani (Rej. Ufafanuzi wa Mt. 19:9, Biblia ya Iringa).

โ€ขJibu 2: Tangu mwanzo wa Kanisa,Aya hiyo yamaanisha Yesu hakuruhusu kupeana TALAKA Bali aliruhusu utengano wa wanandoa bila ruhusa ya kufunga ndoa na mtu mwingine (Rej. Ufafanuzi wa Mt.19:9, Biblia ya Iringa).

Jibu 3: Neno 'Uasherati' kwa kipindi Cha Sasa lamaanisha uzinzi au kukamatwa katika ugoni. Neno ' Uasherati ' kwa kipindi Cha Yesu lilikuwa na maana kadhaa . Mojawapo ni Uhusiano wa kindoa baina ya Maharimu (ndugu wa Damu)- (Rej . R.E. Brown ed.all., NJBC 42 (1990), 643). Uhusiano huu ni haramu pia katika AK (Walawi 18:6-23). Hivyo basi, Hadi Leo Kanisa linaruhusu TALAKA kwa Maharimu.

โ€ขNyongeza: Mk 10:11-12 Yesu mwenyewe anasisitiza kuhusu talaka akisema "kila mtu atakayemwacha mkewe na kumwoa mwingine azini juu yake; na mke akimwacha mumewe na kuolewa na mwingine azini." Rwebangira (talk) 20:11, 2 March 2023 (UTC)[reply]

KUHUSU KUWANYIMA BAADHI YA WAKATOLIKI MAZISHI YA KIKRISTO

[edit]

Shutuma: Wakatoliki wanawanyima mazishi ya Kikristo wenzao, Hii sio haki.

Anayepewa huduma stahiki ya mazishi kama Mkatoliki,ni yule aliyeuishi vizuri ukristo wake. Aliyejitahidi kuzishika vizuri amri za Mungu na za Kanisa katika uhai wake. Ambao hawapewi maziko stahiki ya Kikristo kama Wakatoliki,ni wale ambao hawakuonyesha DALILI yoyote ya kujutia dhambi zao walipokuwa hai, na ambao walikuwa: (i) Waasi dini sugu au wazushi (ii) Ambao kwasababu zao binafsi walitaka miili yao ichomwe baada ya kufa (Rej. Ds 1864-in the "Degree of Holy Office, 15/10/1886"). (iii) Ambao wana dhambi za wazi wazi kiasi kwamba kuwapa mazishi stahiki ni kuleta makwazo kwa waamini.

HITIMISHO: Kumuombea marehemu mazishi ya Kikristo, ni jambo lenye busara kama katika uhai wake; marehemu alitimiza vyema wajibu wake kwa Mungu na Kwa Kanisa. Atapewa haki yake inayompasa, nayo ni maziko stahiki. Lakini kama marehemu hakutimiza wajibu wake vyema kwa Mungu na Kwa Kanisa ili kujipatia wokovu; Kanisa linaheshimu uhuru wa mtu huyo (Rejea Yoh 3:18, 12:48; Mt 12:32, 1Kor 3:12-15), hivyo basi, Kanisa haliwezi kumlazimishia marehemu mazishi halali ya Kikristo. Rwebangira (talk) 20:34, 2 March 2023 (UTC)[reply]

If this is the first article that you have created, you may want to read the guide to writing your first article.

You may want to consider using the Article Wizard to help you create articles.

A tag has been placed on User:Rwebangira requesting that it be speedily deleted from Wikipedia. This has been done under section G12 of the criteria for speedy deletion, because the page appears to be an unambiguous copyright infringement. This page appears to be a direct copy from https://www.facebook.com/MalkiawaRozariTakatifu/posts/pfbid02dBugDNDu7UvrJUsQ7fFFdbBTUNnji2oxdpUWHxd9MaCLan3kxEPdpQM1hrFDuZaUl?__cft__[0]=AZVikV4Kq8fqTY5ykcOHsH1xyencgNYqORcxXIG1rvBy3_e0ZXPLrzkljop8vUkK0ItLzVigH5Zx3p06uV7gEnTTxj1LbYEwGvs70Ya6NbLZgUzmCVBMJjZm-pi9NksZHGixnFL-DMZ0NhpNFdsrdttC0vHT4huCUZXaY9Rkcb9rOKEZKEYsc6tNuWKPY9jSQ4QcYt74oDwFB6e8JSf7qZGq&__tn__=%2CO%2CP-R. For legal reasons, we cannot accept copyrighted text or images taken from other web sites or printed material, and as a consequence, your addition will most likely be deleted. You may use external websites or other printed material as a source of information, but not as a source of sentences. This part is crucial: say it in your own words. Wikipedia takes copyright violations very seriously and persistent violators will be blocked from editing.

If the external website or image belongs to you, and you want to allow Wikipedia to use the text or image โ€” which means allowing other people to use it for any reason โ€” then you must verify that externally by one of the processes explained at Wikipedia:Donating copyrighted materials. The same holds if you are not the owner but have their permission. If you are not the owner and do not have permission, see Wikipedia:Requesting copyright permission for how you may obtain it. You might want to look at Wikipedia's copyright policy for more details, or ask a question here.

If you think this page should not be deleted for this reason, you may contest the nomination by visiting the page and clicking the button labelled "Contest this speedy deletion". This will give you the opportunity to explain why you believe the page should not be deleted. However, be aware that once a page is tagged for speedy deletion, it may be deleted without delay. Please do not remove the speedy deletion tag from the page yourself, but do not hesitate to add information in line with Wikipedia's policies and guidelines. 49ersBelongInSanFrancisco (talk) 06:46, 3 March 2023 (UTC)[reply]

๐—ญ๐—œ๐—™๐—”๐—›๐—”๐— ๐—จ ๐—ฅ๐—”๐—ก๐—š๐—œ ๐—ญ๐—” ๐—•๐—Ÿ๐—จ๐—˜, ๐—ฃ๐—œ๐—ก๐—ž ๐—ก๐—” ๐—ก๐—ฌ๐—˜๐—จ๐—ฆ๐—œ ๐—ญ๐—œ๐—ก๐—”๐—ญ๐—ข๐—ง๐—จ๐— ๐—œ๐—ž๐—” ๐—ž๐—”๐—ง๐—œ๐—ž๐—” ๐—Ÿ๐—œ๐—ง๐—จ๐—ฅ๐—๐—œ๐—”.

[edit]

Ndugu msomaji wa makala haya, najua umejifunza mengi kuhusu rangi mbalimbali zinazotumika katika Liturjia za Kanisa Katoliki. Na uzuri ni kwamba, wengi wetu sio wageni sana kuhusu rangi nyeupe, kijani, nyekundu na zambarau ambazo ndizo zimekuwa zikitumika sana katika Makanisa yetu, tofauti na hizo rangi tatu nilizozitaja hapo juu.

Ukweli ni kwamba, Mapadre wengi wa Kanisa Katoliki wakati wa sherehe mbalimbali za kidini au vipindi maalumu vya mwaka wa Kanisa, hupenda kuvaa mavazi ya rangi husika ili kuwakilisha siku hiyo.

Mfano: wakati wa Majilio na Kwaresma, Mapadre huvaa mavazi ya rangi ya zambarau kuonesha toba au huzuni. Pia wakati wa Noeli, Pasaka au sherehe mbalimbali za Wakatifu, mara nyingi huvaa mavazi ya rangi nyeupe kuonesha ushindi, furaha au usafi wa moyo. Kadhalika hata wakati wa Ijumaa kuu, Pentekoste au katika kumbukumbu za Wafiadini, hulazimika kuvaa mavazi ya rangi nyekundu kuonesha umwagikaji wa damu au kifo. Na pia katika vipindi vya kawaida vya mwaka wa Kanisa, huvaa mavazi ya rangi ya kijani kuonesha utulivu au amani.

Lakini katika historia ya Kanisa kabla ya rangi hizi, mtu wa kwanza kutumia mfumo wa rangi kwenye Misa au Ibada mbalimbali za Kikatoliki alikuwa Papa Innocent III, ambaye yeye alipitisha rangi nne tu ambazo ni nyeupe, nyekundu, kijani na nyeusi mnamo mwaka 1198 - 1216 ila baadae wakati wa Papa Paulo VI mwaka 1969, naye aliweka rangi zote nne lakini aliondoa rangi nyeusi na kuweka rangi ya zambarau. Ingawa licha ya mabadiliko hayo, rangi nyeusi, blue na pink mpaka sasa bado zinatumika katika baadhi ya Parokia zetu.

1. ๐—•๐—Ÿ๐—จ๐—˜

Hii ni mojawapo ya rangi ambayo hutumika hadi sasa katika Liturjia mbalimbali za Kanisa Katoliki, lakini zaidi utaikuta kwenye sherehe za Bikira Maria tu. Maana rangi hii tangu mwanzo iliwakilisha usafi wa moyo, kama ile rangi nyeupe inavyotumika.

Lakini sio sehemu zote utaiona rangi hii, bali utaikuta zaidi kule Hispania, Mexico na Ufilipino. Na pia kama ukitaka kuiona vizuri, angalia picha nyingi za Mama Bikira Maria, utamuona akiwa amevaa vazi la rangi hii.

Lakini sio sehemu zote utaiona rangi blue ikitumika, bali utaikuta zaidi kule Hispania, Mexico na Ufilipino. Na pia kama ukitaka kuiona vizuri, angalia picha nyingi za Mama Bikira Maria, utamuona akiwa amevaa vazi la rangi hii, na hiyo ndiyo sababu kuu rangi hii kutumika hadi sasa katika sherehe zake.

2. ๐—ฃ๐—œ๐—ก๐—ž

Rangi hii kwa jina lingine hujulikana kama rangi ya Mawaridi, sio mara zote utamuona Padre akivaa vazi la rangi hii. Kwani mara nyingi hutumika kwa mwaka mara mbili tu, hasa katika dominika ya tatu ya Majilio na ile dominika ya nne ya Kwaresma.

Rangi hii inapovaliwa humaanisha furaha, yaani wakati wa Majilio Waamini wanaalikwa wawe na furaha wanapojiandaa kumpokea Mtoto Yesu atakayezaliwa kipindi cha Noeli. Kadhalika pia hata wakati wa Kwaresma licha ya kipindi hicho kuwa cha toba na huzuni juu ya mateso ya Yesu, bado Waamini wanaalikwa wawe na furaha maana muda sio mrefu ukombozi wetu utapatikana kwa njia ya kifo na ufufuko wa Yesu. Na ndio maana Mapadre hulazimika kuvaa rangi hii, ila sio katika Parokia zote wana utaratibu huu.

3. ๐—•๐—Ÿ๐—”๐—–๐—ž(๐—ก๐—ฌ๐—˜๐—จ๐—ฆ๐—œ)

Kikawaida rangi hii ilianza kutumika kabla hata ya mageuzi ya Vatican II, mara zote rangi hii ilikuwa inatumika wakati wa mazishi na huvaliwa mpaka sasa na baadhi ya Mapadre.

Hivyo rangi nyeusi kwa wakati ule ilikuwa ni chaguo halali la mazishi, kabla ya rangi ya zambarau haijaanza kutumika katika Kanisa. Maana rangi hii nyeusi ilihusishwa zaidi na maombolezo tangu Roma ya kale na kiutamaduni huwakilisha kifo. Kwahiyo ni nadra sana kuikuta katika Misa za Novus Ordo (Vatican II) ila bado inaweza kuonekana kwenye Misa za Kilatini (Vatican I).

  • Tumsifu Yesu Kristo..!*

Rwebangira (talk) 18:05, 20 March 2023 (UTC)[reply]